Jumamosi, 25 Novemba 2017

Mpango wa kunusuru magonjwa ya mlipuko waandaliwa Kinondoni

Kituo cha afya Magomeni chini ya uongozi wa Manispaa ya Kinondoni ikishiriki na shirika la Japan, JICA wameandaa mkutano wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa kujikinga na magonjwa ya mlipuko yatokanao na uchafu wa kutonawa vizuri mikono.

Kupitia mradi huo  JICA imejitolea kiasi cha shilingi milioni 53 kwa ajiri ya kuunga mkono katika kuendeleza mradi huo,ambapo lengo lake ni kueleimisha watoaji wa huduma ya afya,Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi,katika kata ya kigogo,tandale,na magomeni na kuhusisha shule 15, vituo vya afya 05vilivyopo ndani ya kata hizo.

Aidha kwa upande wake Mganga mfawidhi Omary Mgangwa kutoka hositali ya magomeni amesema kuwa kila mwaka watoto 2195 wanafariki kutokana na magonjwa hivyo jamii lazima ifuate kanuni za usafi kwa kunawa mikono kwa kila hatua ili kupunguza vifo visivyo vya lazima.

Amesema ili nchi iwe na maendeleo lazima watu wake wawe na afya,na ukosefu wa afya hulitia taifa hasara, lakini pia inapoteza muda mwingi wa kulitumikia taifa.

Hivyo amesema ni vema watu wakaelewa kwamba  ni asilimia 80%ya magonjwa yanayosababishwa na uchafu ikiwamo kipindupindu,tyfod,kichocho,homa ya tumbo

Hakuna maoni: