Jumamosi, 25 Novemba 2017

Matukio ya ukatili yapungua Tanzania

Serikali imesema idadi ya matukio yaliyoripotiwa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa tatizo hilo katika kipindi cha miaka 26 ya maadhisho ya kimataifa ya siku ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassani katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema matukio elfu 56 yaliyoripotiwa na kiwango cha asilimia 40 cha watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia kimeonekana kidogo ukilinganisha na ukubwa wa tatizo na kuwataka wazazi kujenga utamaduni wa kuwakagua watoto,kutoa taarifa kwa kuwa vitendo hivyo ufanywa na watu wa karibu na kwa kificho ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dokta Faustine Ndugulile amesema takwimu zinaonesha asilimia kumi na saba ya watoto wenye umri wa miaka 15 hadi watu wazima wenye umri wa miaka 49 wamefanyiwa ukatili wa kingono ambapo katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali imeweka madawati wa jinsia katika vituo mia 556 vya polisi ili wananchi waweze kutoa taarifa, ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na umoja wa mataifa ili kutafuta namna ya kunza kutoa mfunzo ya ukatili wa jinsia ndani ya jeshi la polisi.

Bibi Anna Kulaya ni Kaimu Mkurugenzi wa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika (WILDAF) ameitaka serikali kuweka mkazo katika kupambaba na tatizo la ukatili wa kijinsia ili kuweza kufanikisha sera ya mageuzi ya viwanda na kilimo kwa kuwa wanawake wamekuwa wakitumia muda mwingi katika migogoro,kupeleka ushahidi katika vyombo vy sheria pamoja na kukimbiza na mimba za utotoni badala ya kuzalisha na kubuni miradi viwanda vidogovidogo ambayo vingesaidia katika kuleta maendeleo.

Hakuna maoni: