Jumamosi, 25 Novemba 2017

Kigaila: Kwanini Bashe hajafikishwa Polisi?

Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amedai kwamba anataarifa Chama Cha Mapinduzi kimechukua polisi na kuwavalisha mavazi ya CCM, huku vijana wa chama hicho wakivalishwa magwanda ya polisi.

Kigaila ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari akifafanua namna ambavyo vijana na wanachama wa CHADEMA wanavyoshambuliwa katika mikutano ya kampeni.

Kigaila amesema kwamba yapo makubaliano CCM waliyokubaliana walipokaa kwenye kikao cha Halmashaurikuu (NEC  kilichofanyika mapema wiki hii ndiyo maana hata viongozi wake wamekuwa wakitoa matamko kwa kujiamini kuhusu kuwashambulia chadema.

Kigaila ameongeza kwamba "CCM wamemaliza kikao cha NEC juzi wametawanyika.

Wanachukua polisi wanawavalisha mavazi ya CCM na wao CCM wamevalishwa mavazi ya polisi na wamewapeleka kwenye Kata. Polisi siyo chombo cha siasa. Wanalipwa kodi za wananchi hivyo hawapswi kutumika katika kumwaga damu za wananchi".

Aidha Kigaila amehoji ni kwa nini Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe hajafikishwa polisi kwa kauli yake mbele ya Mwenezi wa chama hicho (Humphrey Polepole) akihamasisha wana CCM wasisite kuwashughulikia wapinzani kwa kuwa wao wanadola.

"Mambo anayoyasema Bashe ndiyo waliyokubaliana CCM, nataka kumwambia IGP kwamba polisi ni kwa ajili ya kulinda usala wa raia wote. Kwanini Polisi hawajamkata Bashe? Bashe anasema watu wapigwe, alitakiwa awe ameshakamtwa awepo segerea au Central Polisi lakini ametangaza vijana wa CCM wapige watu na baada yapo wakafanya hivyo halafu watu wetu ndiyo wakakamatwa. Damu za watanzani a zitadaiwa mikononi mwa IGP na CCM. Kigaila.

Mbali na hayo Kigaila ameongeza kwamba amemshuhudia Msukuma wakati anatoka Kaskazini maeneo ya Korogwe alikuwa na watu ambao amedai ni Majambazi wanaofahamika huku akidai kwamba alikuwa akitoka kwenye kikao cha NEC.


Hakuna maoni: