Dar es Salaam. Mchezaji wa Simba, John Bocco ndiye anayeongoza kwa kuitia Simba hasara kubwa zaidi kwani katika kipindi hicho cha miezi mitatu, amechukua mishahara inayofikia Sh20 milioni huku akifunga bao moja pekee.
Laudit Mavugo amekuwa na nafuu kwani katika kipindi hicho amelipwa mishahara ya Sh 13.5 milioni na kufunga mabao mawili. Nicholas Gyan ndiye amekula mshahara wa bure kwa kulipwa Sh16.5 milioni huku akiwa hajafunga kabisa.
Juma Liuzio amechukua kiasi cha Sh7.2 milioni na kufunga bao moja tu katika kipindi hicho. Straika huyo wa zamani wa Zesco United ya Zambia hajafunga bao lolote tangu Agosti 26.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni