Jumatano, 22 Novemba 2017

Marekani yatangaza kuwaua magaidi 100 nchini Somalia

Jeshi la Marekani latangaza kuwaua wanamgambo 100 wa kundi la kigaidi la al Qaida  katika kambi ya al Shabaab nchini Somalia.

Jaeshi la Marekani katika kştengo chake kwa ajili ya Afrika limefahamisha kuwa jeshi la anga la Marekani limeshambulia kambi ya wanmagmbo wa al Shabaab inayopatikana katika umbali wa kilomita 200 na jiji la Mogadishu.

Zaidi ya magaidi 100 wa kundi hilo wameuawa katika shambulizi hilo.

Kundi la al Shabaab kwa ushirikiano na kundi la al Qaida na Daesh  yanashukiwa kuendesha shambulizi la bomu mjini Mogadishu na kusababisha maafa makubwa.

Watu zaidi 350 walifariki katika shambulizi hilo lilitokea mjini Mogadishu.

Hakuna maoni: