Jumatano, 22 Novemba 2017

MALISA GJ AZUNGUMZIA TUHUMA KUWA NA YEYE YUPO NJIANI KUIHAMA CHADEMA



baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa MAVICHA bwana Katambi na wanachama wengine wa CHADEMA kukihama chama hicho na  kujiunga na CCM ,kuna  tetesi kuwa Kijana Shupavu wa CHADEMA Ndugu Malisa Gj nae yupo mbioni kukihama chama hicho.

Kufuatia  tetesi hiyo ,Ndugu Malisa Gj ameibuka na kutolea ufafanuzi kwa kuandika ujumbe ufuatao kwenye ukurasa wake wa Instagram

 "Just to make clear on the crap that is going on to the social media. Sijahama. Sihami. Sina mpango wa kuhama. Kitu pekee kinachoweza kushake membership yangu ni kama Chadema itatoka kwenye misingi yake. Si Pesa, si cheo, si vitisho. Infact vitisho nimevizoea, lakini Utu wangu, Imani yangu na Falsafa inayoongoza maisha yangu ni vya muhimu zaidi kuliko fedha au cheo chochote.

Wakati wao wnafikiria pesa na vyeo, mimi namfikiria Lissu, namfikiria Mawazo, namfikiria Ben Saanane. Hawa wananipa kila sababu ya kuendelea kupambana kwa nguvu zaidi. Siwezi kusaliti mapambano waliyoyaasisi. Siwezi kusaliti damu zao.

Kwa miaka mingi Chadema imekua tumaini la wanyonge. Wakati huu watanzania wanahitaji watu majasiri wanaoweza kuwatetea bila woga, kuliko wakati mwingine wowote. Kukimbia mapambano ktk kipindi hiki ni kusaliti watanzania waliotuamini. Dhambi hiyo ni kubwa sana. Siwezi kuifanya.

Malisa GJ"
 


Hakuna maoni: