Msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shabani ‘Keisha’.
Akipiga stori na Full Shangwe Keisha alisema, anatarajia kurudi kwa kishindo hivi punde kwenye gemu lakini kazi yake haina uhusiano wowote na kusambaa kwa picha za harusi ya Dogo Janja na Uwoya bali watu wanamzushia tu. “Ni kweli narudi kwenye muziki lakini ujio wangu hauna uhusiano kwa namna yoyote ile na kusambaa kwa picha za harusi za Janjaro na Uwoya.
Mimi ni Muislamu safi, kamwe nisingeweza kukubali kuhusisha mambo matakatifu ya dini na vitu vya kidunia, watu waache kuzusha kuwa ni maandalizi ya video yangu mpya,”alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni