Jumanne, 7 Novemba 2017

Bosi wa Chelsea kuachia ngazi, Conte tumbo joto

England. Mkurugenzi wa bechi la ufundi klabu ya Chelsea, Michael Emenalo ameacha kazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 10.

Taarifa hiyo huenda ikawa ni mbaya zaidi kwa Kocha Antonio Conte ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa kwa uongozi wa klabu hiyo kuhusu kuendela kuwapo kwenye klabu hiyo.

Emenalo amekuwa akihudumu kwenye timu hiyo kama mkurugenzi wa benchi la ufundi na sasa anatarajiwa kujiunga na mabingwa wa Ufaransa, Monaco.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo alisema sababu za kuachia nafasi hiyo ni kutokana na masuala ya kifamilia, huku akisema zaidi anataka kuwalea vyema watoto wake.

Hakuna maoni: