Ijumaa, 20 Oktoba 2017

Vimezinduliwa vifaa vipya kwaajili ya zimamoto na maafa Dsm

 Wadau mbalimbali wanaounganika pamoja kwaajili ya kukabalina na majanga  Jijini Dar es salaam (Dar MAERT) Wamezindua mpango na kukabidhi vifaa vya mawasilianio wakati wa dharura na maafa ili kukabiliana na majanga ya moto katika jiji hilo kitaalamu na kwa haraka.
Mfumo huo uliozinduliwa na mkuu wa wilaya ya kigamboni Hashim Mgandilwa kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, umeunganisha magari yote zimamoto na ya dharura yaliyo katika vituo vyote kwenye mfumo mmoja ambayo itakuwa ni rahisi katika kuwasiliana.
Katika taarifa ya mkoa, DC Mgandilwa amesema ni matarajio ya wlio wengi kuwa mpango huo utakuwa mwarobaini wa majanga yanayotokea Jijini humo. Ambapo licha ya kuahidi kuendelea kutenga bajeti pia ameagiza watakao kabidhiwa vifaa hivyo wahakikishe vinatumika kwajili ya maafa tu na sio vinginevyo.

Kwa upande wake mratibu wa Wadau mbalimbali wanaounganika pamoja kwaajili ya kukabalina na majanga (DARMAT) Dkt Christopher Mzava, amemueleza mgeni rasmi kuwa licha ya uhaba wa vifaa vya kuzimia moto na uokoaji pia kukosekana kwa mifumo ambayo inaelekeza namna ya ukoaji bora ilikuwa ni changamoto kubwa na kwamba kuzinduliwa kwa mfumo huo utasaidia kukabiliana na majanga kitaalamu.
Jiji la Dar es salaam linahitaji Vituo 20 vya zimamoto lakini kwsasa vipo 4, halikadhalika tuna magari 6 tu ya kubebea wagonjwa wa dharura. Aliongeza.

Hata hivyo mkurugenzi wa idara ya maafa  kutoka ofisi ya waziri mkuu Brigedia Mbazi msuya ameshauri Dar MAERT kushirikiana na watu binafsi wanaomiliki Magari ya huduma za dharura kwa kusajili magari yao ili kukabiliana na changamoto hiyo, na ameahidi kushirikiana na wadau hao.
Mpango huo umefadhiliwa na benki ya dunia, na kwamba ufadhili huo ni kufuatia kuongezeka kwa changamoto za majanga ya moto na maafa katika jiji hilo.


Hakuna maoni: