Tanzania imeendelea kushuka kwenye viwango vya soka duniani baada ya leo shiriksho la soka la kimataifa FIFA kutoa viwango vya mwezi Oktoba ambapo Tanzani imeporomoka kwa nafasi 11.
Katika Kalenda ya FIFA ya mwezi Oktoba Tanzania ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi Oktoba 7 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kutoa sare ya bao 1-1, Tanzania ikitokea nyuma na kusawazisha.
Viwango hivyo vya leo vinaonesha Tanzania imeporomoka kwa nafasi 11 kutoka nafasi ya 125 kwa mwezi Septemba hadi nafasi ya136 mwezi Oktoba.
Uganda ambayo ilitoa sare ya 0-0 dhidi ya Ghana imepanda kwa nafasi moja kutoka 71 hadi 70 na kuendelea kuongoza kwa viwango kwa upande wa Afrika Mashariki. Kenya imeshuka kwa nafasi 14 kutoka nafasi ya 88 hadi 102.
Katika orodha ya jumla Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno na Argentina wakati Tunisia ikiongoza kwa Afrika ikiwa nafasi ya 28 baada ya kupanda kwa nafasi tatu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni