Jumapili, 1 Oktoba 2017
Sina tofauti na Juma Nature nikiwa jukwaani - Ney Wa Mitego
Msanii Ney Wa Mitego, amefunguka na kusema kuwa yeye ni msanii ambaye anafanana na mkongwe Juma Nature kwa kupata mapokeo makubwa pamoja na kushangiliwa zaidi wakati akiwa jukwaani.
Ney amezunguza kwa kueleza kuwa yeye anapokuwa hajapanda jukwaani kwa ajiri ya ‘Show’ kitu kikubwa ambacho huwa anafanya kusali kwanza na baada ya kumaliza huwa anasali kitu ambacho anaamini kuwa kinamsaidia sana yeye na kuweza kupata mapokeo makubwa katika maonesho yake mbalimbali kutokana na kumtanguliza Mungu.
‘’Mi situmii ndumba kabisa na kitu ambcho huwa nakifanya kabla ya kupanda jukwaani mi huwa nasali na nikimaliza kufanya ‘Show’ vilevile huwa nasali pia kitu ambacho kinanifanya mimi niwe napata mapokeo makubwa na kufanya ‘Show’ ambazo zinakuwa na shwange nyingi’’ amesema Ney.
Hata hivyo, mkali huyo anayefanya vizuri na wimbo wake wa Acheze ameongeza kuwa kutokana na shangwe ambazo amekuwa anazipata kwenye ‘Show’ zake ni sawa na zile ambazo amekuwa akipata msanii mkongwe wa muziki huu wa Bongo Flave Juma Nature.
Ney ni msanii ambaye amekuwa hataki kukaa kimya hasa katika utoaji wa nyimbo na nyimbo zake nyingi ambazo amekuwa akizitoa zimekuwa zikipata mapokeo na mafanikio makubwa na wakati mwingine kuwashangaza mashabiki wake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni