Ijumaa, 6 Oktoba 2017

Beki kisiki wa zamani wa Chelsea, Real Madrid ahukumiwa kwenda jela miezi saba

Beki wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Ricardo Carvalho amehukumiwa kwenda jela miezi saba.

Carvalho ameonekana alikwepa kodi na kuhukumiwa kwenda jela miezi saba nchini Hispania.

Beki huyo aliyeichezea Chelsea na pia mechi 89 timu yake ya taifa ya Ureno, anaonekana atafanya kila linalowezekana kukata rufaa.

Hispania imekuwa nchi inayoonyesha kutotaka utani katika suala la ulipaji kodi.

Hakuna maoni: