Jumapili, 22 Oktoba 2017

Alikiba atambulisha aliyomshirikisha G Nako

Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' ameitambulisha rasmi 'Cover' ya wimbo wake huo ambayo imefanya na rapa G Nako Wara Wara kutoka katika kundi la WEUSI.

Alikiba wakati anaitambulisha ngoma hiyo iliyofanywa na G Nako amesema kuwa ni moja kati ya nyimbo zake zilizorudiwa na kutokea kuipenda sana kwani anadai G Nako ameitende haki sana kazi yake hiyo.

Wakali hao wote wawili wamekuwa wakionekana kwenye majukwaa kadhaa wakiimba pamoja wimbo huo kwa namna tofauti na kupokelewa vizuri na mashabiki zao jambo lililompelekea G Nako kurudi wimbo mzima.

Hakuna maoni: