Jumatatu, 25 Septemba 2017

STARKE AONGEZWA KIKOSI CHA BAYERN


Faridi Miraji, Dar es salaam.                          


Mabingwa wa Bundesliga klabu ya  Bayern Munich imemjumuisha kikosini mlinda mlango Tom Starke katika kikosi kinachoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mwaka 2017/18 kuziba pengo la mlinda mlango Manuel Neuer ambaye ni Majeruhi.

Sheria za UEFA zinaruhusu mlinda mlango kuongezwa au kuondolea kikosini katika hatua ya makundi ya mashindano hayo, Hivyo Bayern watakuwa na walinda mlango watatu akiwemo Starke, akiungana na mlinda mlango  Sven Ulreich na  Christian Früchtl ambao wote wamejumuisha katika kikosi  kitakachowavaa  Paris Saint-Germain jumatano hii.

Starke ni nani? 
Uenda likawa jina geni kwa wapenzi wengi wa soka lakini Tom Peter Starke ni raia wa Ujerumani akizaliwa Machi 18, 1981.

== kuhusu Klabu ==

Starke amecheza  Bayern Munich kwa mara ya Kwanza Octoba 31,2012 katika finali ya DFB-Pokal dhidi ya FC Kaiserslautern na pia alicheza mchezo wake wa kwanza wa Bundesliga dhidi ya TSG 1899 Hoffenheim Machi 3,2013.

Starke alitundikia daruga mwishoni mwa msimu uliopita, na amekuwa akiendelea kujifua na kikosi cha Bayern Munich na alishiriki katika michezo ya maandalizi ya msimu huu mpya (Pre -season )akiwa na Bavarian.


Hakuna maoni: