Faridi Miraji , Dar es salaam.
Mchezaji nyota wa Real Madrid na timu ya taifa Ureno Cristiano Ronaldo, amefikisha mechi 400 katika klabu yake ya Real Madrid.
Ronaldo amefikisha idadi hiyo ya kuichezea klabu hiyo hapo jana dhidi ya Borussia Dortmund katika Michuano ya klabu bingwa barani ulaya UEFA, huku akifanikiwa kufunga magoli mawili kati ya matatu na lingine likifungwa na mchezaji mwenzake Gareth Bale, na kuilaza Borussia Dortmund Kwa goli 3-1.
Ronaldo, ameichezea klabu hiyo ya Real Madrid mechi 400 akifunga magoli 411 na msaada (Assists) 111 pamoja na kufunga magoli matatu (Hat Trick) 42.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni