Jumapili, 24 Septemba 2017

NAIROBI HOSPITAL:HATUJAPOKEA PESA KUTOKA BUNGE LA TANZANIA KWA AJILI YA MATIBABU YA LISSU


Hospitali ya Nairobi alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha wanasheria nchini Tundu Lissu imesema haijapokea fedha zozote kutoka bunge la Tanzania hadi kufikia jana saa 10 jioni. Mkuu wa mahusiano ya umma wa KHA inayomiliki hospitali hiyo Bi.Catherine Njoroge ameiambia televisheni ya K24 kwamba hadi kufikia jana malipo hayo yalikuwa hayajafika kwenye akaunti yao.

Catherine alieleza hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji wa K24 aliyetaka kujua kama wamepokea malipo hayo ya TZS 43Milioni sawa na Shilingi 2.1Milioni za Kenya, baada ya bunge la Tanzania kueleza kuwa limefanya malipo hayo tangu jumatano ya tarehe 20 mwezi huu.

"Akaunti iliyotajwa kwenye taarifa ya bunge la Tanzania ni sahihi, lakini bado fedha hizo hazijafika. Kama walituma kwa TT (Telegraphic Transfer) muamala huchukua hadi saa 48 kukamilika. Hivyo kama kweli walituma tunategemea kufikia jumatatu fedha hizo zitakua zimeonekana kwenye akaunti" alisema Catherine.


Hakuna maoni: