Akiwa mkoani Tanga Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa Ado Shaibu amewaeleza Viongozi wa ACT Wazalendo Mkoani humo
Kuwa hadi sasa Chama hicho hakina kundi lolote kwenye mzozo wa CUF kwakuwa Hadi sasa hakuna kikao kilichoketi na kuazimia kuwa wako wa Maalim Seif au wa Profesa Lipumba.
Ameeleza kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia maswali kadhaa kutoka kwa wanachama wao kutaka kujua msimamo wa chama juu ya mgogoro huo ambapo aliongeza kuwa wanaamini kuwa mambo ya ndani ya CUF yatamalizwa na Wana-CUF wenyewe. Si sahihi kwa Chama kingine cha siasa, iwe ACT, iwe Chadema au CCM kudhani kuwa chenyewe kitakuwa mwarobaini wa kuitibu CUF.
"Kwa hiyo msimamo wa Chama Chetu ni kutoingilia mambo ya ndani ya CUF, Jambo pekee tunaloweza kufanya ni kushauri ili kutekeleza wajibu wetu wa kupigania demokrasia. Mara kadhaa tumefanya hivyo. Ndugu Zitto na Chama kwa nyakati tofauti kimewahi kuwataka Wana CUF kuridhiana. Wana CUF wana chaguo wao wenyewe kuupokea au kuutupa ushauri huo." Aliongeza Ado Shaibu
Aidha ameeleza kuwa Chama cha ACT-Wazalendo kiliundwa na Watu waliochoshwa na mizengwe na kukosekana kwa demokrasia ya ndani kwenye vyama vyao vya awali na hivyo ameshauri waendelee kutoa fursa kwa wapiganaji wa kila Chama, wasio na vyama na kutoka kila kundi ambao wamechoshwa na mizengwe wapaone ACT kuwa eneo salama la kufanya siasa na mapambano ya kiukombozi.
"Na Kama tunavyorudia mara kwa mara, viongozi mujikite kufanya siasa za masuala. Jitengeni kwenye porojo. Pazeni sauti kwa ajili ya shida za watu. Tikifanya hivi. Kila mmoja atatupenda na tutakuwa tumetimiza ndoto yetu ya kuwa Chama mbadala wa uhakika." Alisema Ado Shaibu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni