https://www.facebook.com/ZAKABOYBLOG/
Umewahi kufanya biashara kisha biashara ikafa na kupata hasara? Je, uliwahi kujiuliza ni biashara imefirisika au wewe umejifirisi (umefirisi) biashara?
Mara nyingi biashara haiwezi ku collapse over night. Ni process yaani inaanza kutoa viashiria kidogo kidogo mpaka mwisho ina meet natural death.
Kwa mfanyabiashara makini ni lazima ajifunze:
1. Kuepuka viashiria vya kufilisika biashara
2. Kugundua viashiria hivyo
3. Kutafsiri viashiria hivyo.
2. Kugundua viashiria hivyo
3. Kutafsiri viashiria hivyo.
Ni muhimu kujua kuwa viashiria vya kucollapse biashara vinatoka ndani na nje. Vishiria vya nje ni kama vile:
1.Kupungua kwa mauzo/wateja kutokana na soko kutokuwa zuri hivyo biashara kutofanya vizuri.
2.Kuongezeka kwa kodi (pango,TRA,Leseni nk) kiasi cha kufanya matumizi kuwa makubwa pengine kuliko mauzo. Hii hasa ni kwa biashara ndogo au inayoanza
2.Kuongezeka kwa kodi (pango,TRA,Leseni nk) kiasi cha kufanya matumizi kuwa makubwa pengine kuliko mauzo. Hii hasa ni kwa biashara ndogo au inayoanza
Mara nyingi viashiria hivi vya nje ni rahisi kuvigundua na kuvichukulia hatua stahiki.
Sasa tuangalia viashiria vya ndani ambavyo kwa kiasi kikubwa ndivyo vinapelekea biashara kufa. Mara nyingi hivi husababishwa na mwenyebiashara. Ikumbukwe kuwa ipo tofauti kubwa kati yabiashara na mwenyebiashara. Mara nyingi mwenyebiashara anapoingilia biashara basi kuna uwezekano mkubwa wa kudorora kwa biashara na hatimae biashara kufa.
Mfano:
1. Kuikopa biashara bila mwenyebiashara kuilipa biashara. Hapa ni pale unapochukua unga, sabuni, sukari kwenye duka lako bila kulipa. Mbaya zaidi hata kuandika kuwa ulikopa huandiki kwa vile tu wewe ndie mwenye biashara.
1. Kuikopa biashara bila mwenyebiashara kuilipa biashara. Hapa ni pale unapochukua unga, sabuni, sukari kwenye duka lako bila kulipa. Mbaya zaidi hata kuandika kuwa ulikopa huandiki kwa vile tu wewe ndie mwenye biashara.
2. Kutoweka rekodi za biashara. Mfano: kutopiga hesabu kila silu, wiki, mwezi nk. Yani unafanya tu biashara kiholela, hujui stutus ya biashara yako ikoje.
3. Kufanya matumizi yasiyo ya lazima ndani ya biashara. Mfano kuingiza mzigo mpya wakati wa zamani haujauza, unafanya hivyo ili tu shelf za duka zisionekane tupu (mbavu za mbwa), au unanunua gari la kutembelea kwa pesa ya biashara ,wakati kumbe kwa wakati huo ulitakiwa uendelee kupanda daladala kwenda kwenye biashara yako kwa sababu hali ya biashara haijawa nzuri kukuruhusu kununua gari.
4. Kutokujilipa mshahara/posho. Wewe unaihudumia biashara ,hivyo ni sehemu ya wafanyakazi wa biashara, unatakiwa ujilipe posho au mshahara kiasi utakachoamua kwa kuzingatia Hali halisi ya biashara. Wengi hawajilipi matokeo yake anaona kama hakuna faida anayopata ,hivyo anachofanya ni kudokoa kodogo kidogo kwenye mtaji akodhani ndio njia ya kujilipa kutokana na faida anayopata.
5. Kufanya biashara kimazoea! Hapa mfanyabiashara anaweza akawa anafungua au kufunga duka kwa mfano muda wowote anaojisikia, bila kujua kuwa kufanya hivyo ni kupoteza wateja. Pia kukopesha wateja kimazoea kama vile ndugu, au rafiki ambapo mwisho wa siki anashindwa kuwadai na inakuwa imekula kwake, hatimae anakuwa ameifilisi biashara.