Ijumaa, 5 Januari 2018
Watu 37 wafariki kwa mafuriko na maporomoko ya udongo
Watu 37 wamefariki dunia kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamikia Alhamisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, serikali imesema.
“Siyo tu kwamba kulikuwa na mafuriko, bali pia maporomoko ya udongo, kuzolewa kwa baadhi ya nyumba na mto kujaa maji kupita kiasi,” amesema Waziri wa Afya na huduma za jamii, Dominique Weloli.
Miongoni mwa waliofariki dunia Waziri Weloli alisema ni “watoto wawili au watatu waliozama katika kitongoji cha Bandal”. Kwa mujibu wa redio Okapi, watoto watano wa familia moja walisombwa na maji wakiwa usingizini katika kitongoji hicho hicho.
Lakini mvua zimeathiri zaidi vijiji vya eneo la milimani la Ngaliema ambako vimeripotiwa vifo 13 na Selembao vifo tisa.
Mafuriko ni maafa makubwa yanayowakumba wakazi wa Kinshasa, mji wenye vurumai ukikaliwa na watu wapatao 10 milioni, wengi wao wakiwa masikini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni