mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akizungumza na wananchi wa Kilolo waishio jijini Dar es Salaam leo
Wana Kilolo waishio Dar wakiwa katika kikao cha maendeleo na viongozi wa Kilolo leo
Mkuu wa wilaya ya Kilolo akifurahia jambo leo
Picha za matukio ya wana Kilolo waishio Dar
Akizungumza leo katika kikao cha pamoja kilichofanyika Magomeni jijini Dar es Salaam mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa wilaya hiyo imepiga hatua kubwa katika sekta mbali mbali zikiwemo za viwanda ,Afya ,Kilimo ,elimu na sekta nyingine nyingi na hivyo kuna haja ya wanaKilolo kuwa wa kwanza kufika kuwekeza zaidi katika wilaya hiyo .
“ Tumefanikiwa kupiga hatua kubwa katika sekta mbali mbali kama hili la viwanda tayari Kilolo tunaviwanda vimeanza vikiwemo vya nyanya na viwanda vingine huku kiwanda cha Chai Kidabaga kipo mbioni kufufuliwa “
Pia alisema kwa upande wa utalii wilaya ya Kilolo imebarikiwa na kuwa na vivutio vingine vya utalii ila shida iliyopo ni kukosekana kwa hoteli za kitalii na hivyo kupitia kikao hicho iwe fursa kwa wanaKilolo waishio Dar es Salaam na nje ya Kilolo kufika kuwekeza katika sekta ya utalii .
“ Toka nimefika Kilolo nimekuwa nikitembelea vivutio mbali mbali vya utalii kweli tunavyo vingi na vizuri sana naombeni sana turudi kuwekeza nyumbani ili muweze kuwekeza katika sekta hii ya utalii “
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mafanikio mbali mbali ya kimaendeleo katika wilaya hiyo yamekuwa yakipatiokana kutokana na ushirikiano kati yake mbunge na mkurugenzi pamoja na wananchi wa wilaya ya Kilolo.
Kwani alisema katika kuifanya ofisi yake kuwa ni ofisi rafiki kwa wananchi ametoa ruksa kwa mwananchi yeyote mwenye uhitaji wa kuonana na mkuu wa wilaya kufika ofisini kwake wakati wowote ila kwa kufikisha mambo ya kimaendeleo na sio majungu kwani ofisi yake haipokei majungu .
Kwa upande wake mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto akielezea utekelezaji wa Ilani katika wilaya ya Kilolo alisema kuwa wamefanikiwa kufanya vizuri katika elimu na kuwa wilaya hiyo ilikuwa nyuma zaidi katika elimu ila sasa ndio wilaya inayoongoza kwa ufaulishaji wa wanafunzi wa kidato cha sita .
Kuhusu sekta ya maji alisema upo mradi mkubwa wa maji Ilula unaendelea kujengwa pia kila kata kuna mradi wa maji unajengwa wakati umeme kwa kata zote zitapata mwaka huu isipo kuwa katika kata mbili pekee.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi aliwataka wana Kilolo kucjhangamkia fursa zilizopo katika wilaya hiyo na kuwa tayari viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vimepimwa .
Mkurugenzi huyo alisema kuwa wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ambayo zao la Parachichi na Korosho zinakubali na hivyo ni lazima wananchi hasa wanaoishi nchi ya Kilolo kurudi kuwekeza katika kilimo hicho.
Mdau wa maendeleo Danford Mbilinyi ambae pia ni mkurugenzi wa Umoja Switch alisema alisema ni jambo la kushangaza sana kuona kijana wa Kilolo analalamika kukosa pesa wakati kuna ardhi inayofaa zaidi kwa kilimo cha miti na hivyo wanayo nafasi ya kulima miti ambayo itawasaidia kiuchumi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni