Jumamosi, 6 Januari 2018

Wakulima waiomba Serikali iingilie kati mgogoro wa ardhi Morogoro

Wakulima wa kijiji cha Kimamba A na B wilayani kilosa mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuingilia kati mgororo wa ardhi katika shamba ambalo linadaiwa kutelekezwa na mwekezaji na baadae kurudishwa kwenye halmashauri ya Kilosa .

Ombi hilo kwa serikali limekuja kufuatia kuzuka kwa mgogoro wa maeneo ya kilimo katika shamba la kimamba estate na kueleza uwepo wa mvutano kutokana na vijiji vya malangali na Mabwelebwele kuzuia wakulima wakijiji cha kimamba kulima katika shamba hilo ambalo wanadai walikua wakilitumia kwa muda mrefu na baadaye likarudishwa kwenye halimashauri ya kilosa .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amesema kuwa jitihada za kutosha zinafanyika ili kuhakikisha wakulima wa kimamba wanapata maeneo ya kilimo hivyo viongozi wa vijiji wanatakiwa kupeleka majina ya wananchi ambao hawana maeneo ya kulima.

Hakuna maoni: