Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kunusurika katika machimbo yasiyo rasmi eneo la Nzuguni manispaa ya Dodoma baada ya machimbo hayo kufurika maji kutokana na mvua kubwa.
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika manispaa ya Dodoma zimeleta maafa baada ya mashimo ya wachimbaji hao kugharikishwa na maji ya mvua hali iliyopelekea mchimbaji mmoja kupoteza maisha.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhandisi Dr Binilith Mahenge, ametoa pole kwa familia ya wafiwa na kuagiza kufungwa mara moja kwa machimbo hayo kwani hayapo kisheria na ni hatari kwa maisha ya wakazi wa eneo hilo.
(Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Giles Muroto amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mwili wa marehemu ulipokuwa unaopolewa na ametoa wito kwa wananchi kuvunja nyumba zilizopo eneo hilo linalomilikiwa na polisi na kusitisha shughuli za uchimbaji).
Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji manispaa ya Dodoma Amiri Issa, amesema kwa ushrikiano na wananchi imewachukua masaa 10 kufanikisha kutolewa kwa marehemu ndani ya shimo akiwa tayari ameshafariki.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni