Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam imetenga takribani shilingi bilioni moja na milioni mia moja, kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na wanawake.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Ubungo Bi. Rose Andrew amesema pesa hizo zitatolewa kupitia vikundi vya wafanyabiashara na wajasiriamali vitavyoundwa na vijana pamoja na wanawake katika manispaa hiyo.
Aidha Bi. Andrew ameongeza kuwa mikopo hiyo itaanza kutoka hivi karibuni na kuwataka wakazi wa Ubungo wachangamkie fursa hiyo inayotokana na ahadi ya serikali ya kuwawezesha wananchi wake kiuchumi.
Kwa upande mwingine Bi. Andrew amesema tayari fomu za maombi ya mikopo hiyo zimeshapelekwa kwa maofisa maendeleo ya jamii kwenye kata zote 18 za Manispaa hiyo.
Afisa maendeleo huyo amemaliza kwa kusema kuwa kipaumbele katika kupata mikopo hiyo kitatolewa kwenye biashara zinazofanywa kwenye maeneo rasmi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni