Alhamisi, 11 Januari 2018

SINGIDA UNITED WANAUNGANA NA YANGA KESHO KUPANDA BOTI YA KURUDI BARA



Timu ya Singida united itaungana na yanga kesho kupanda Azam marine na kurejea Tanzania bara baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya mapinduzi usiku huu.

Singida wameondolewa kwenye michuano hiyo katika hatua ya nusu fainali, mchezo uliopigwa usiku huu dhidi ya Azam Fc na Azam kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani wa aina yeke ulimalizwa na mchezaji wa Azam,Iddy Chilunda aliyefunga goli hilo pekee   kunako dakika ya 78.

Hii ni nusu fainali ya pili baada ya ile ya mapema kati ya URA na Yanga ambapo URA waliibuka na ushidi kwa njia ya penaiti.

Mchezo wa fainali kati ya URA na Azam utachezwa tarehe 13 Januari,2018 ambayo ni siku ya Jumapili


Hakuna maoni: