Mhariri wa BBC nchini China Carrie Gracie amejiuzulu kutoka wadhifa wake akilalamikia kutokuwepo usawa wa mshahara na wafanyakazi wenzake wa kiume.
Kwenye barua Bi Gracie ambaye amefanya kazi na BBC kwa zaidi ya miaka 30, ameilaumu BBC kwa ubaguzi katika malipo.
Alisema kuwa BBC inakumbwa na tatizo la kuaminiwa baada kufichuliwa kuiwa thuluthi mbili ya manyota wanaolipwa zaidi ya pauni 150,000 walikuwa ni wanaume.
BBC inaasema kuwa hakuna ubaguzi dhidi ya wanawake.
Bi Gracie alisema kuwa aliwaacha wadhifa wake kama mhariri wa ofisi ya Bejijing wiki iliyopita lakini bado atasalia BBC.
Alisema atarudi kwa wadhifa wake wa zamani katika chumba cha habari cha televisheni ambapo anatarajiwa kulipwa sawa na wengine.
Bi Gracie alisema alishangazwa kugundua kuwa wahariri wawili wa kiume wa kimataifa wa BBC, walilipwa asilimia 50 zaidi kuliko wenzao wawili wa kike.
Mhariri wa Marekani Jon Sopel analipwa kati ya pauni 200,000-249,999, huku mhariri wa Mashariki ya Kati Jeremy Bowen naye analipwa kati ya pauni 150,000-199,999.
Gracie hakuwa katika orodha hiyo ikimaanisha kuwa mshahara wake ulikuwa chini ya pauni 150,000.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni