Jumanne, 16 Januari 2018
Man City kuachana na mpango wa kumsajili Sanchez
Ripoti kutoka nchini England zimeeleza kuwa klabu ya Manchester City imeamua kuachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez ambaye imekuwa ikimwinda kwa muda mrefu.
Meneja wa vinara hao wa ligi kuu soka nchini humo Pep Guardiola amekutana na mmiliki wa klabu hiyo Khaldoon al Mubarak na viongozi wengine na kukubaliana kuachana na usajili huo wa Sanchez mwenye umri wa miaka 29.
Moja ya sababu kubwa ambayo imeeleza kusababisha timu hiyo kujitoa kwenye mbio hizo ni mshahara mnono ambao Sanchez amehitaji kulipwa ambao ungemfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi ndani ya kikosi hicho kitu ambacho viongozi wameona sio sawa.
Kwa upande wake kocha Jose Mourinho wa Manchester United akizungumza baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke City jana usiku amesema, hapaswi kuzungumzia suala la Sanchez kwasababu ni mchezaji wa Arsenal.
"Sanchez ni mchezaji wa Arsenal, kama atabaki itakuwa nzuri kwa Arsenal, kama atakuja kwetu itakuwa ni nzuri kwetu na hata kama ataenda klabu nyingine itakuwa ni nzuri kwao''.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni