Mwalimu Oluoch ambaye ni muumini wa kanisa la Waadventista wasabato alifungua shauri hilo dhidi ya Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye kupitia tangazo maalumu la serikali aliitangaza siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku maalumu ya kufanya usafi kitaifa.
Mahakama kuu imekubaliana na maombi ya Mwalimu Oluoch na kumruhusu kutoshiriki usafi katika siku hiyo ya jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa kuwa tangazo husika linaingilia haki yake ya kuabudu kinyume na ibara ya 19(1) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hivyo mahakama ilikataa ombi la kuitaka mahakama iiamuru serikali kuitangaza siku ya Jumapili ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi kwa waumini wa SDA kama alivyoomba Mwalimu Oluoch kwa sababu moja, shauri hilo halikufunguliwa kwa ajili ya kuwawakilisha Waumini wengine wa SDA (Representative suit) pili, mahakama haina mamlaka ya kuiamuru serikali kufanya hivyo.
Hivyo mahakama imempa kibali Mwalimu Oluoch kutoshiriki siku ya usafi ya siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kwani inaingilia Uhuru wake wa kuabudu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni