Jumatano, 10 Januari 2018

Kauli ya Olesendeka yamuamsha Spika Ndugai

Spika wa Bunge Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili na kuchunguza kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka inayodaiwa kudhalilisha bunge.

Hatua hizo za Mh. Spika zimekuja baada ya kauli zinazodhaniwa kuwa ni za Mh. Olesendeka zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge ambazo zilikuwa zikitamkwa kwa Lugha ya Kimasai, kiswahili na Kingereza.

Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari imesema kwamba , Spika ameelekeza kuwa Kamati hiyo  imuite na kumhoji Kiongozi huyo  ikiwa ni pamoja na kuchunguza ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.

Kauli zinazodaiwa kuwa ni za Ole- Sendeka zilisikika zikisema kwa  'bunge limemomonyolewa'.




Hakuna maoni: