Mwaka 2012 kocha wa Manchester City Roberto Mancini alitajwa kama kocha aliye kwenye nafasi kubwa kumchukua Robin Van Persie, lakini katika hali isiyoeleweka RVP alikwenda kukipiga Manchester United.
Kitendo cha Robin Van Persie kujiunga na Manchester United kinatajwa kwamba kilikuwa tatizo kubwa kwa mabosi wa Manchester City na ilionekana Mancini hana ushawishi kwa wachezaji wakubwa ndio maana wakamtimua.
Lakini Mancini kwa kipindi kile hata hakuwa tatizo bali tatizo lilikuwa Manchester City, RVP alikuwa amecheza kwa muda EPL lakini hakuwa amebeba kombe hivyo sio pesa tu bali pia alihitaji na kombe.
Manchester City na Manchester United walimuahidi Van Persie kiwango cha pesa kisichotofautiana sana lakini ilimbidi Van Persie kuangalia kitu cha ziada katika vilabu hivyo ndipo akaamua kwenda United.
2012 Manchester United walikuwa wametoka kubeba makombe 4 kati ya 6 yaliyopita ya EPL, wakatoka kucheza fainali ya Champions League na huku kocha wao ni Sir Alex Ferguson, Van Persie angekataaje pesa na faida zote hizi?
Miaka karibia 6 imepita tangu Robin Van Persie akutane na suala hilo na sasa kumeibuka movie lingine linalofanana na la Van Persie lakini safari hii muhusika mkubwa akiwa ni Alexis Sanchez huku United na City wakiwa vitani.
Mimi sio malaika kujua nini kipo kichwani mwa Sanchez lakini haihitaji kuwa malaika kufahamu kwamba Sanchez anaidai EPL, tangu amekuja amekuwa katika kiwango cha hali ya juu lakink hajawahi kubeba kombe.
Sanchez anaweza kufanya kile alichofanya Van Persie lakini akafanya kwa utofauti, atakwenda Manchester City. Haitakuwa rahisi kwa Ed Woodward na Mourinho kukataliwa lakini pia haitakuwa ngumu kwa Sanchez kutaka kuungana tena na Pep Gurdiola.
Sio tu uzuri wa kikosi cha Pep Gurdiola ndio utamvutia Sanchez, bali pia Pep na Sanchez wana historia ndani ya Barcelona na vile vile mshahara mnono ndani ya City vitamshawishi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni