HERI ZA MWAKA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MARAFIKI WA MAISHA YA USHINDI {2}
BWANA YESU asifiwe.
Tunaelekea kusherekea ukumbusho wa kuja kwa ukombozi duniani maana hakuna uzima popote ila ni kwa YESU KRISTO {Yohana 14:6,YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. }.
=Ndio maana dunia nzima ni shangwe na furaha kwa tukio ambalo limetokea miaka zaidi ya 2000 iliyopita ambapo siku YESU anazaliwa malaika ambao ni jeshi la mbinguni walishangilia na kumsifu sana MUNGU
{Luka 2:8-14,Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa BWANA akawatokea ghafula, utukufu wa BWANA ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo BWANA. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu MUNGU, na kusema,Atukuzwe MUNGU juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. }
Siku hiyo hiyo YESU mwanaume wa ajabu anazaliwa watu wenye heshima na watawala walimsujudia
{Mathayo 2:11, Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. }
hao walijua kuwa aliyezaliwa ni MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana.
Pia YESU alizaliwa kwenye hori la ng'ombe ashilio la kwamba wanyama wapumzike maana hakuna tena sadaka ya kuteketezwa kama ilivyokuwa zamani maana YESU ni dhabihu idumuyo milele ili watu wasamehe dhambi zao na kuurithi uzima wa milele bure kupitia yeye {Waebrania 9:12-15, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake KRISTO, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa MUNGU kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu MUNGU aliye hai? Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. }.
Naitwa Zakaboy nawatakia mwaka mpya mwema mfike sarama katika safari yenu
Tafadhali andika coment jina la mtu wako ma3 nami nitazipeperusha santeni nyote
Maoni 3 :
Saramu zangu zimefikia popote alipo Ndungu masumbuko Mfaume
By Mtz media group
Good sana wadau big up kwa sapoti
Good sana
Chapisha Maoni