Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Sigmar Gabriel ameionya Marekani juu ya hatari ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv na kuupeleka Jerusalem akisema hatua hiyo haitapunguza mgogoro uliopo, bali itazidi kuuchochea zaidi.
Onyo hilo la Sigmar Gabriel linatolewa baada ya Rais Donald Trump kusema atauhamisha ubalozi huo na kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas aliyearifiwa na Trump kuhusiana na mipango ya kuuhamisha ubalozi huo amesema hatua hiyo itasababisha madhara katika ukanda huo na duniani kwa ujumla.
Ikulu ya Marekani-White House imesema Rais Trump atatoa tamko kuhusiana na suala hilo leo ambapo Jumuiya ya kimataifa haijawahi kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, lakini maafisa wa Israel wamekuwa wakiushawishi utawala wa Trump kufanya hivyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni