Na Shaban Khamis,Mtilah Blog
Kati ya tarehe 21,22 na 23 Disemba kila mwaka ni siku maalumu ambayo wachina husherehekea kuukaribisha msimu wa baridi kwa lugha ya kichina huitwa (冬至),Dong zhi.
Ni siku ambayo hushiriki pamoja kuandaa chakula maalumu kiitwacho "jiaozi" na kula pamoja.
Leo Dismba 22, 2017 Walimu na wanafunzi wa Chuo kikuu cha waislamu Morgoro wameshiriki pamoja na walimu raia wa China waliopo chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo.
Katika sherehe hizo,walimu wachina ambao wapo chuoni hapo kufundisha Lugha ya Kichina chini ya taaisisi ya Confucious, waliwafundisha wanafunzi wa chuoni hapo namana ya kuandaa Chakula cha kichina "Jiaozi" ambacho ni msingi wa Sherehe hiyo na kula pamoja.
Licha ya chakula hicho,pia kulikuwa na maonesho ya michezo mbalimbali ya kichina.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Makamu mkuu wa Chuo ,Prof.Hamza Njozi ambae katika hotuba yake aliwasisitiza na kuwashauri wanafunzi kutumia vizuri fursa iliyopo chuoni hapo ya kujifunza Lugha ya Kichina.
Pia Pro.Njozi alisema wanafunzi wa MUM ambao wanasoma Lugha ya kichina wamekuwa wakifanya Vizuri kila mwaka na ndio chuo kinachoongoza Tanzania kupeleka wanafunzi wake wengi nchini china kwa ajili ya kujiendeleza zaidi.
Kulia Prof.Hamza Njozi ,Kushoto Mr.Zhang
Kwa upande wake mkuu wa taasisi ya Confucious Chuoni hapao,Mr Zhang alianza kwa kuwakaribisha watu wote kushiriki pamoja kwenye shughuli hiyo,pia alitoa pongezi kwa uongozi wa chuo kwa kuleta Lugha ya kichina ndani ya chuo hicho.
Chuo kuu cha waislamu Morogoro ni miongoni mwa vyuo nchini ambavyo vinafundishs Lugha ya Kichina. Kichina kilianza kufundishwa chuoni hapo mwaka 2012 chini ya usimamizi wa taaisi ya kichina ya Conficious.
Kila mwaka Chuo hupeleka wanafunzi ncini China ambao wanafanya vizuri katika masomo yao.
ZIFUATAZO NI PICHA ZA MATUKIOMBALIMBALI
Wanafunzi na walimu wakishiriki pamoja kuandaa "Jiozi"
Jiozi zikiwa Tayari
Kulia,Mwanafunzi wa MUM akiimba shairi maalumu la Kichina
Mkuu wa kitivo cha sayansi na sanaa ya Jamii,Dr Salim akitoa Neno
Mr.Zhang anampa zawadi maalumu Pr.Hamza Njozi
Mr.Zhang anamuaga Prof Njozi baada ya shughuli kumalizika
Kushoto (Mwenye T-shirt Nyeusi),Mkurgenzi wa Mtlha Blog,Karim Mtila akiwa na Mtangazaji wa Radio MUM FM,Ndugu Majd.Walikuwepo kwenye sherehe hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni