Jumatano, 6 Desemba 2017

Mourinho aanza chokochoko dhidi ya Gurdiola

Mwishoni mwa wiki hii dunia itasimama, mchezo mkubwa kabisa wa kufunga mwaka EPL utapigea kati ya majirani wawili Manchester United watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester City.

Huu ni mchezo baina ya vilabu viwili vyenye nguvu ya pesa lakini pia ni mchezo kati ya makocha wawili ambao wanatajwa kuwa moja kati ya makocha bora sana duniani katika kizazi cha sasa.

Kama kawaida Jose Mourinho na Pep Gurdiola mara zote maneno hayakosekani, tayari Jose Mourinho ameanza maneno kwa kumshutumu kocha wa Manchester City Pep Gurdiola kwamba anadanganya kuhusu majeruhi.

Gurdiola alinukuliwa akisema kwamba David Silva ni majeruhi na anaweza kukosa mchezo wa Derby, jambo hilo limepokelewa tofauti na Mourinho kwani anaamini sio kweli na Pep anajua kwamba Silva atakuwepo.

Mourinho amedai kwamba yeye kwa upande wake hawezi kusema uongo hata siku moja kuhusu majeruhi, na majeruhi wote ambao Mourinho alisema awali hawatakuwepo katika kikosi hicho hawatakuwepo kweli.

United wanakutana na City ambao msimu huu wanaonekana kuwa tishia kubwa si tu nchini Uingereza bali barani Ulaya kwa ujumla, kama City atashinda mchezo huu atazidi ongeza pengo la alama kati yake na United na United wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo.

Hakuna maoni: