Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameitaka halmashauri ya jiji la Arusha kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo vyake vya ndani ili kuchochea kasi ya shughuli za maendeleo katika Jiji hilo ambalo idadi ya watu wake imetajwa kuongezeka kwa kasi kutokana na muingiliano mkubwa wa watu wa kada mbalimbali.
Gambo anatoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Arusha ambayo inatarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya laki nne kutoka wilayani humo na maeneo ya jirani ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanasababisha hospitali ya mkoa ya mountmeru kuelemewa.
Gambo anasema kwa sasa mapato yanayokusanywa na jiji la Arusha kwa mwaka bado hayatoshelezi hata kulipa mishahara ya watumishi wake na kwa maana hiyo ni muhimu kuweka mifumo thabiti ya ukusanyaji wa mapato jijini humo.
Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya arusha kwa awamu ya kwanza unafanyika katika moja ya maeneo ya wazi yaliyo kuwa yakimilikiwa kinyemelela na baadhi ya wajanja wachache na kwa sasa ujenzi umeanza ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 500 hii ikiwa ni jengo la Ghorofa moja kwa ajili ya wagonjwa wa nje.
Ujenzi wa Hospitali hiyo unatarajiwa kukamilika June mwaka 2018 ambapo zaidi ya wakazi laki 4 watapata huduma ya afya karibu na makazi yao tofauti na ilivyo sasa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni