Mkutano wa kwanza wa kuandaa kuwarudisha nyumbani wahamiaji kutoka Libya umeanza ambapo viongozi wa Umoja wa Afrika wanakutana na washirika wake, EU, UNHCR na Shirikisho la Kimataifa la linaloshughulikia masuala ya wahamiaji (IOM), mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.
Taasisi hizo zinakutana kujadili namna ya kuwarejesha nyumbani wahamiaji wanaoendelea kukabiliwa na hali nzito nchini Libya.
Mkutano huo unafuatia video iliorushwa na kituo cha televisheni cha CNN kuhusu kuuzwa kwa wahamiaji kama watumwa, hali ambayo ilisababisha mgawanyiko wa kisiasa na kidiplomasia kati ya baadhi ya nchi za Afrika na Libya.
Umoja wa Afrika, kama taasisi zingine, tangu wakati huo unaonyesha nia ya kuhamasisha ili kusaidia wahamiaji wanaoendelea kukabiliwa na hali nzito nchini Libya kutafutiwa ufumbuzi wa kuondokana na khadhia hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni