Ijumaa, 22 Desemba 2017

MADHARA YA KUNYWA MAJI BARIDI BAADA YA KUMALIZA KULA






Mtu anapokunywa maji baridi mara baada ya kula chakula, maji yale yanapopita kwenye utumbo huchangia kugandisha mafuta yaliyomo kwenye chakula.

Kitendo hicho, husababisha usagaji wa chakula kuwa wa taratibu sana na hivyo kuchangia ukosefu wa choo. Mbali na ukosefu wa choo, ambao ni madhara yanayojionesha kwa muda mfupi, lakini pia kuna madhara ya muda mrefu yanayoweza kujitokeza baadaye sana.

Inaelezwa zaidi kuwa, wakati chakula kinapochelewa kusagwa kwa sababu ya kuganda kulikosababishwa na maji baridi, chakula hicho hukutana na 'acid' iliyoko tumboni ambayo huanza kuyayusha mafuta hayo haraka na kufyonzwa na utumbo kabla ya chakula chenyewe.

Hali hii inapoendelea kwa muda mrefu, tabaka la mafuta (fats) hujijenga kwenye utumbo na baadaye huweza kusababisha saratani ya utumbo.

Halikadhalika, huweza kuwa chanzo kingine cha ugonjwa wa moyo ambao madhara yake ni pamoja na kupatwa na Kiharusi na hatimaye kifo.

Ili kuepuka hatari hii, unachotakiwa kufanya ni kuacha tabia ya kunywa maji baridi na badala yake pendelea kunywa maji ya uvugu-vugu mara baada ya kula chakula.

Vile vile zingatia ushauri wa kukaa kwa muda usiopungua nusu saa ndiyo unywe maji.


Hakuna maoni: