Viongozi wa makundi ya whatsApp (Group Admins) karibuni watapewa uwezo mkubwa wa kudhibiti wanachama wa makundi yao kuweza kuzuia au kufuta ujumbe utakaotumwa katika makundi yao.
WhatsApp imekusudia kuleta maboresho ya kipengele hicho baada ya maombi ya watumiaji wengi kuomba kuwe na kipengele cha namna hiyo kwa muda mrefu.
Maboresho hayo yanatarajiwa kuwepo kwa watumiaji wote wa WhatsApp katika siku za usoni na tayari kwa watumiaji wa toleo la whatsApp beta kwenye baadhi ya nchi wameanza kupata kipengele hicho kwa majaribio .
Ni kwamba maboresho hayo yatamuwezesha kiongozi wa kundi la WhatsApp kuzuia ujumbe wa mwanachama kuonekana katika kundi mpaka atakapoidhinisha uonekane katika kundi zima au anaweza kuruhusu ujumbe uonekane na kama ataona kuna haja ya kuufuta basi anaweza kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya WABetaInfo ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu kila kipengele kipya kutoka WhatsApp ni kwamba kiongozi wa kundi anaweza kuzuia au kufuta Picha za mnato, Video, Documents, GIF, Ujumbe wa Sauti na ujumbe wa maneno.
Maboresho kwenye WhatsApp: Kiongozi wa kundi anaweza kuweka mpangilio katika kundi lake kwamba hakuna atakayeweza kutuma chochote katika kundi mpaka pale yeye atakaporuhusu kufanya hivyo.
Vilevile kiongozi wa kundi anaweza kuruhusu yeyote kutuma lakini akaweza kufuta kama ataona kilichotumwa kipo kinyume na taratibu za kundi.
Kipengele hicho kinafafana na kile kilichopo katika makundi ya Facebook ambapo kiongozi wa kundi anaweza kuzuia ujumbe kutoonekana kwa wanakundi wengine mpaka aidhinishe yeye au kufuta kilichotumwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni