Jumanne, 19 Desemba 2017

Korosho zisizo na ubora kufukuza wanunuzi Lindi

Zaidi ya tani miatatu za Korosho ghafi kutoka chama kikuu cha ushirika Lindi mwambao zimekosa soko kutokana na kukosa ubora unaostaili hali inayotishia kufukuza wanunuzi wa zao hilo ambao wengi wanatoka nje ya nchi.

Hilo limejitokeza katika mnada wa nane wa Korosho uliyofanyika katika kata ya kiwalala lindi vijijini ambapo tani elfu moja na arobaini za korosho ghafi ziliuzwa huku baadhi ya maghala korosho zake zikishinea kununuliwa kutokana na kukosa ubora.
 
Akizungumza katika mnada huo Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao Omar Selemani amesema ghala la Nangurukulu lililokuwa na Korosho tani miamoja na mbili zimekuosa soko kutokana na kukosa ubora, huku ghala la buko lililokuwa na korosho tani mianne na kumi, tani miambili tu ndiyo zimepata soko.
 
Kufuatia hilo amevitaka vyama vidogo vidogo vya wakulima amcos  kutopokea korosho zisizo na ubora kutoka kwa wakulima kwani zinaathiri soko la zao hilo.
 
Kwa upande wake meneja wa chama kikuu cha Lindi Mwambao Hassani Rashidi amesema kuuza Korosho zisizo na ubora athari yake ni kubwa ikiwemo kufukuza wanunuzi ambao wengi wanatoka nje ya nchi, huku meneja rasilimali watu na utawala kutoka bodi ya Korosho Tanzania shauri mokiwa amesema wakulima lazima wabadilike vinginevyo wataendelea kupata hasara na kukosa soko kabisa la zao hilo.


Hakuna maoni: