Jumatatu, 4 Desemba 2017

Hawa ndio magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea

Arsenal walishambulia lango la Manchester United mara 15 Jumamosi, lakini hawakufanikiwa kutikisa wavu isipookuwa mara moja tu - kikwazo chao David de Gea.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alisema uchezaji wa golikipa huyo wake ulikuwa "bora zaidi duniani".

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia alikiri kwamba Mhispania huyo alciheza kwa ustadi mkubwa na kwamba "alikuwa ndiye mchezaji bora wa mechi kwa mbali sana".

Uchezaji wake ulikuwa muhimu sana kwani uliwasaidia kulaza Arsenal 3-1 - na pia ulifikia rekodi Ligi ya Premia.

Buffon achukua nafasi ya Neuer kikosi bora cha Fifa

Hatua yake ya kuzima makombora 14 inamfanya kushikilia rekodi ya kuzuia makombora mengi zaidi mechi moja Ligi Kuu England pwa pamoja na mlindalango wa zamani wa Newcastle Tim Krul na kipa wa zamani wa Sunderland Vito Mannone.

Waliozuia makombora mengi zaidi mechi moja EPL tangu Agosti 2003 (Opta walipoanza kufuatilia data)
Tarehe Timu Mchezaji Mpinzani Aliokoa
19 Apr 2014 Sunderland Vito Mannone Chelsea 14
2 Des 2017 Man Utd David de Gea Arsenal 14
10 Nov 2013 Newcastle Tim Krul Tottenham 14
21 Mar 2015 West Brom Boaz Myhill Man City 13
7 Nov 2004 Fulham Mark Crossley Newcastle 13
2 Jan 2017 Sunderland Vito Mannone Liverpool 13
28 Feb 2016 Swansea Lukasz Fabianksi Tottenham 13
8 Apr 2006 Man City David James Tottenham 13


Hakuna maoni: