Chuo kikuu cha Dar es salaam
Chuo kishiriki cha Mkwawa
Iringa
06/12/2017.
Kwa yeyote Mdau wa Elimu Tanzania,
YAH. MSAADA WA KUNISAIDIA NIENDELEE NA MASOMO YANGU
Ninaitwa GRACE S. MUSSA ninasoma Shahada ya Elimu katika Chuo kikuu cha Mkwawa (Iringa) Mwaka wa kwanza. Kwa bahati mbaya mimi ni yatima (sina wazazi wakuweza kughalimia masomo yangu). Hata Elimu ya Sekondari na nimesoma kwa msaada wa Halmashauri ya wilaya Kibondo-Kigoma na TASAF.
Kwa bahati mbaya zaidi, baada ya kufaulu kujiunga na Chuo kikuu niliona kama ndoto zinakuja kutimia, lakini mbaya zaidi nimeomba mkopo sijabahatika kupangiwa mkopo kwa awamu zote, nikashauriwa nikate rufaa lakni bado nimekosa. Nipo Chuo yapata Mwezi sasa sijafanya Usajiri ila huruma ya Uongozi wa Chuo ulinivumilia mpaka majina ya rufaa yatoke, sasa yametoka na sijabahatika tena . (Inauma sana). (sijui niende wapi)
Kwa barua hii, ndugu watanzania wenzangu, wazazi, viongozi wa serikali na Dini naomba msaada wenu, nimefanya kila juhudi kuhakikisha Napata Mkopo lakini kila juhudi hazizai matunda.
Naomba kwa yeyote anayeguswa na shida yangu hii usambaze barua yangu mpaka imufikie mtetezi wa kuweza kunisemea niweza kutimiza ndoto yangu ya kulijenga taifa na kumtetea mtoto wa Kike mwenzangu aliyefungwa na tamaduni na tabia za jamii yetu.
Naomba vyombo vya habari (redio na magazeti), mitandao ya kijamii na mtu mmoja mmoja unisaidie kusambaza hili.
Inauma saana unapoongeza juhudi kujikwamua lakini inatokea nguvu nje ya uwezo wako inakurudisha kwenye taabu na mateso, kama una huruma tafadhari sambaza ujumbe huu
Kwa mawasiliano yangu: 0766277709,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni