Jumapili, 12 Novemba 2017

Wenger kumsajili Zaha

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amepanga kumsajili winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha kuziba pengo la Alexis Sanchez, kwa mujibu wa habari.

Gunners wameshindwa kumzuia mshambuliaji wao kuondoka majira ya joto, kwani hajasaini mkataba mpya na yupo tayari kufanya mazungumzo na klabu nyingine Januari.

Wenger alikuwa na tumaini la kumpata winga wa Monaco Thomas Lemar dirisha la uhamisho wa majira ya joto, lakini dili hilo lilishindikana, lakini The Sun limedai kuwa Mfaransa huyo atarudi kumfukuzia mchezaji huyo.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Zaha amefurahia mwanzo wa msimu huu akiwa amefunga magoli mawili katika mechi tano alizocheza 2017-18.

Ripoti zinadai kuwa Arsenal wapo tayari kutoa paundi milioni 35 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, ambaye ndio kwanza amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Tottenham kuonyesha nia ya kumsajili.

Hakuna maoni: