Inawezekana watu wengi wanajiuliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba atakuwa upande gani kwenye mechi ya VPL kesho kati ya Singida United dhidi ya Yanga?
Waziri Nchemba anajulikana ni shabiki ‘lialia’ wa Yanga kwa sababu mara kadhaa ameonekana akiisapoti timu hiyo ndani na nje ya uwanja lakini pia siku za hivi karibuni amekuwa bega kwa bega na klabu ya Singida United.
http://ift.tt/1vJep6E imemnasa Waziri Nchemba kwenye exclusive na amesema kesho Jumamosi ya November 4, 2017 atakuwa upande gani wakati timu hizo mbili zitakapokutana (Singida United vs Yanga).
“Nilikuwa naonekana Yanga wakati Singida bado haipo ligi kuu, lakini kama unafuatilia tangu Singida irejee ligi kuu nimekuwa nikiisapoti mara zote”-Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
“Kesho itakuwa ni nyumbani kwanza, nitakuwa Singida United nikiungana na mashabiki wengine wa hapa nyumbani kuishangilia timu yetu.”
“Kwa mara ya kwanza Singida United itakuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa Namfua tangu ligi ianze, tulikuwa tunatumia uwanja wa Jamhuri Dodoma lakini baada ya ukarabati kukamilika tumerejea nyumbani.”
Jambo kubwa la hivi karibuni ambalo mashabiki wa Yanga wanalikumbuka kutoka kwa Waziri Nchemba ni namna alivyomshawishi kocha Hans kurejea kwenye timu baada ya kocha huyo kujiuzulu kufuatia tetesi za ujio wa George Lwandamina kuchukua nafasi ya Hans.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni