Jumanne, 14 Novemba 2017
Walimu manispaa ya Kinondoni kupewa tuzo
Manispaa ya Kinondoni imefanya vizuri zaidi katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017 kwa kupata ufaulu wa asilimia 93.02, ambapo imekuwa halmashauri ya kwanza kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari meya mstahiki wa kinondoni Benjamin Sitta amesema kuwa jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ni 11,701 huku wavulana wakiwa 5,589 na wasichanaa ni 6,129, waliofanya ni 11,701 kati ya hao waliofaulu ni 10,884.
Aidha kutokana na mafnikio hayo manispaa ya Kinondoni kwa kutambua mchango wa walimu imeamua kutoa tuzo kwa walimu wote ambao masomo yao yamefanya vizuri kwa kufaulisha alama "A", hivyo kila A moja mwalimu wa somo husika atapewa sh.2500 ikiwa ni mwanzo na motisha kwa walimu.
Hivyo shule zote 78 zilizopata ufaulu wa juu kwa mwaka 2017 zitapewa tuzo ili kuzihimiza shule zote kuongeza juhudi na kuimarisha ufaulu wao kwa kasi zaidi.
Kutokana na mafanikio hayo manispaa ya Kinondoni imeamua kuandaa hafla yakutoa tuzo hizo ambapo itazinduliwa kiwilaya tarehe 15/11/ mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Msingi Mbuyuni na baadae tarehe 18 novemba kila kata watakaa pamoja kati ya viongozi wa kata, mtaa na wajumbe wa kamati ili kupanga na kutatua changamoto za elimu zilizopo.
" Nachukua fursa hii kuwapongeza walimu wote wa shule za msingi, wazazi mkurugenzi, afisa elimu na Rais kwa jitihada anazozifanya kwa kufanikisha mpango wa elimu bure ambapo unapelekea kupata matunda haya" alisema Sitta.
Hivyo kwa wote walioalikwa katika hafla waweze kuhudhulia ili kuwapongeza walimu kwa ngazi ngazi zote za wilaya na kata.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni