Wafugaji wamemuomba waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina kuingilia kati tofauti iliyopo kati ya wafugaji na serekali ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa madai ya kuonewa dhidi ya kukamatwa kwa mifugo yao.
Ombi hilo limekuja baada ya serikali ya Mvomero mkoani Morogoro kukamata Ngíombe 209 wanaodaiwa kuchungwa katika kijiji cha magali kata ya melela kinyume cha sheria huku ngíombe zaidi ya 40 wakipakiwa kwenye maroli chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi kwa ajili ya kwenda kupigwa mnada ambapo o baadhi ya wafugaji wameeleza kuwa mifugo hiyo ilikamatwa ndani ya zizi kisha kuswagwa na mgambo kwa madai kuwa ilikuwa mashamban.
Akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamedi Utali amekili kukamatwa kwa ngombe 209 katika kijiji cha magali na kueleza kuwa walikuwa wakiharibu vyanzo vya maji na mazao ya wakulima baada ya hatua za kisheria ngombe 40 watapigwa mnada kufidia faini ya makaosa yao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni