Mapunye ni aina ya magonjwa ambayo hushambulia zaidi sehemu ya kichwani mwa binadamu.
Mapunye husamba kwa kasi kubwa kwa njia zifuatazo;
1. Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususan pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hao.
2. Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari .
3. Kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo.
Watu ambao huweza kupata maambukizi ya mapunye ni wafuatao:
1. Wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri.
2. Wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo.
3. Wanaotoka jasho hasa kichwani kwani huweza kuweka mazingira mazuri zaidi kuruhusu maambukizi yatokee kirahisi.
4. Wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu.
5. Wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia.
6. Wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea.
7. Wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kufanya usafi wa kichwa.
8. Watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kinga ikiwamo kisukari.
9. Wale wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibayotiki) kwa muda mrefu.
10.Watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.
Jinsi ya kuyatambua ugonjwa huu.
Mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili.
Matibabu
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.Matibabu ya mapunye huchukua muda mfupi kuonyesha matokeo mazuri.
Kama nilivyoandika kwenye makala zilizopita matibabu ya fangasi huleta matokeo chanya mara zote, ila pia huwa ni rahisi kwa maradhi hayo kurudi baada ya kumaliza matibabu kama hatua madhubuti za kujikinga na maradhi haya hazitochukuliwa.
Kwa sababu hiyo, ni vizuri kwa mgonjwa wa fangasi kutumia dawa mpaka wiki mbili baada ya dalili za maradhi kutoweka.
Jinsi ya kujikinga na mapunye
Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na fangasi:
1. Hakikisha mwili wako hasa kichwani yanabaki na ukavu muda wote
2. Osha nguo, taulo na mashuka kuhakikisha fangasi wanaondolewa
3. Epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalum ya kuua vimelea kabla hujatumia.
4. Epuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au uweke dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni