Jumatano, 8 Novemba 2017

UDART yaahidi kurejesha huduma katika hali ya kawaida Kesho

Watoaji wa huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini dar es salaam UDART wamemweleza Naibu waziri ofisi ya rais – TAMISEMI Josephat Kandege kuwa wanataraji kurejesha huduma katika hali ya kawaida kesho , mara baada ya kukamilisha taratibu za utoaji wa vifaa vya kutengenezea magari yaliyoathirika na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwezi uliopita na kuparaganyisha usafiri katika barabara ya morogoro eneo la jangwani daraja la msimbazi.

Maelezo hayo yametolewa na mkurugenzi mtendaji UDART CHARLES NEWE baada ya naibu Waziri Kandege kutembelea mradi huo kwa lengo la kuangalia utendeji kazi wake hususan changamoto zinazowakabili watoa huduma na wasafiri, ambapo ameelezea kifaa kilichoharibika katika mabasi yapatayo 28 kiitwacho VOITH kinachowezesha kubadilisha gia za gari kimeagizwa nje ya nchi na tayari kimeingia hapa nchini kinachonedelea sasa ni taratibu za kutoa mzigo huo bandarini huku gharama za kutengeneza basi moja zikitajwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 8.

Naibu waziri Kandege ameanzia safari yake kituo cha kivukoni na baadae kituo cha kikuu cha mabasi hayo Jangwani ambapo amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kifupi ambacho mabasi yanafanyiwa matengenezo kwani hali hii haikuweza kuzuilika.

Hata hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhali hususan wakati wa misimu ya mvua ambazo husasabisha athari katika maeneo mbalimbali ya miji huku akisisitiza kuwa hata waendeshaji wa kituo hicho wanatakiwa kujihadhali kwani eneo hilo si zuri nyakati za mvua na ndio maana serikali imeshauri mabasi yanayolala katika kituo hicho kuhamishiwa kituo cha gerezani kwa kuepuka gharama na usalama zaidi.

Hakuna maoni: