Jumatano, 8 Novemba 2017

Tembo wavamia , wauwa na kuharibu mazao

Wimbi la tembo limeibuka na kuharibu mazao ya wakulima wa baadhi ya vijiji vya kata ya Kiwangwa , Mkange na Kibindu vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Saadan na vilivyo karibu na Mto Wami .

Watu watatu wanadaiwa kuuawa kutokana na wanyamapori hao ambapo kati ya watu hao wawili wamefariki baada ya kujeruhiwa na fisi katika kijiji cha Kiwangwa na mtu mwingine alikufa kutokana na kujeruhiwa na tembo huko kwa Kwamduma.

“Tembo wameharibu mazao hekari zaidi ya 200, kifo cha mtu mmoja kilichosababishwa na tembo na vifo viwili vilivyotoka na fisi, Idara husika imepata taarifa na ilisema ipo sheria ya kulipa kifuta jasho walioathiriwa ama kuuawa na wanyamapori”. Amesema diwani kata ya Kiwangwa, Malota Kwaga
Akitoa taarifa hiyo kwenye kikao cha madiwani cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ngazi ya kata kipindi cha robo mwaka ,diwani wa kata ya Kiwangwa Malota Kwaga ,amesema tembo wamekuwa tatizo na kutishia maisha ya watu .

Hakuna maoni: