Nyota wa klabu ya Diffaa El Jadida ya Morocco Simon Msuva ambaye anaichezea timu ya taifa ya Tanzania amewaomba Watanzania kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars, huku akiahidi kujituma zaidi ili kutowaangusha mashabiki.
Akiongea leo asubuhi kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Msuva amesema, mashabiki waendelee kuipa nguvu timu hiyo na wao kama wachezaji watajitahidi kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
“Mashabiki waendelee kuiunga mkono taifa stars kwani ndio timu yao na sisi kama mashabiki tutajituma kupata matokeo mazuri ili tuwafurahishe”, amesema Msuva.
Naye nahodha wa Taifa Stars Himid Mao Mkami amesema kuwa wameshatazama video za timu ya taifa ya Benin na wamejipanga vyema kwenda kuikabili na kuibuka na ushindi siku ya mchezo huo Novemba 12.
Taifa Stars inaondoka kesho alfajiri kuelekea nchini Benin kwaajili ya mchezo huo wa kalenda ya shirikisho la soka la kimataifa FIFA ambapo itakuwa bila ya nyota wake wa kimataifa nahodha Mbwana Samatta na Farid Mussa ambao ni majeruhi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni