ARUSHA. Timu Singida United yenye makao yake makuu mjini Singida imeipiga mkwara mzito watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga dhidi ya tambo zake za matumaini ya kuvuna pointi tatu katika Uwanja wa Namfua keshokutwa Jumamosi.
Singida inatarajia kuwakaribisha wageni wao, Yanga katika uwanja wake wa nyumbani katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu zinazoendelea, huku Yanga wakitoa tambo za uhakika wa kuvuna pointi tatu dhidi ya Singida United ili kuwa vinara wa Ligi Kuu.
Timu ya Singida united inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm iko katika kiwango kizuri huku mwalimu huyo akichukulia mechi hiyo ya kawaida sana kutokana na kuwajua wachezaji wa klabu yake ya zamani.
Katibu Mkuu wa Singida United, Abrahmani Sima amesema kuwa timu yake tiyari iko imara kuwakabili Yanga, hivyo wanafanya mazoezi ya mwisho mwisho kwa ajili ya maandalizi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni