SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa mpango kazi wa taifa katika kutokomeza ukatili dhidi ya mtoto kwa kupunguza mimba na ndoa za utotoni kwa asilimia 27.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,Mkurugenzi wa maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Margaret Mussai katika kongamano la watoto wakike lililoandaliwa na jukwaa la utu wa mtoto (CDF).
Amesema kua,Serikali imekua ikifanya juhudi mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini ili kutimiza lengo la watoto kielimu pamoja na kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shirika hilo, Koshuma Mtengeti amesema kuwa ,lengo la kongamano hilo ni kuwapatia fursa watoto wa kike katika utekelezaji wa miradi inayofanywa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na kutokomeza ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.
Aidha ameongeza kuwa, shirika la CDF limekuwa likiwasaidia watoto wa kike waliofanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiri amali ili kuweza kujikwamua na hali duni ya maisha pamoja na kuondokana na utegemezi katika jamii
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni